COSTECH Integrated Repository

Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa

Show simple item record

dc.creator Tandiko, Neema
dc.date 2019-08-20T06:19:21Z
dc.date 2019-08-20T06:19:21Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:35Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:35Z
dc.identifier Tandiko, N. (2015). Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/970
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/970
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulichunguza dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa, uliongozwa na malengo matatu ambayo ni: kuchunguza namna taswira zinavyojitokeza katika nahau za Kisambaa, kuchunguza athari zinazojitokeza katika matumizi ya taswira katika kufafanua na uelewekaji wa nahau za Kisambaa kwa hadhira pamoja na kutathimini uhusiano uliopo baina ya taswira zipatikanazo katika nahau za Kisambaa na maisha halisi ya jamii. Mapengo yaliyojitokeza katika kutoa msukumo wa kufanya utafiti huu ni haya; Kwanza, wengi wa wataalam hao wamezishughulikia nahau kwa kuzikusanya na kuangalia maudhui yake kama walivyotajwa katika usuli wa tatizo la utafiti, hata hivyo, hawakukishughulikia kipengele cha taswira. Pili, uchunguzi wao umejigeza katika nahau za Kiswahili na lugha nyingine lakini sio lugha ya Kisambaa. Mbinu ya udodosaji, mahojiano na mjadala wa vikundi zilitumika katika kukusanya data. Mbinu ya ufafanuzi ilitumika ambapo mkabala wa Umuundoleo ulitumika katika uchambuzi wa data.Vitongoji vitatu pamoja na Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa vilihusishwa katika kuwakilisha watafitiwa. Matokeo ya utafiti yanabaini kuwa nahau za Kisambaa zimeenea katika vipengele mbalimbali vya maisha ya jamii hiyo. Nahau zilizochambuliwa zinaakisi mazingira yanayoihusu jamii hiyo pamoja na vitu vitumikavyo katika jamii husika. Mchango mpya ambao umeibuliwa katika utafiti huu ni kukuza ufahamu juu ya matumizi ya taswira katika Fasihi, hususani katika kipengele cha fani ambapo taswira chomozi katika nahau za kisambaa zimeelezwa kama sehemu ya taaluma katika Fasihi simulizi ya Kiswahili.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Dhima
dc.subject Taswira
dc.subject Dhima ya taswira
dc.subject Nahau
dc.subject Nahau za Kisambaa
dc.subject Kisambaa
dc.subject Fani
dc.subject Semi
dc.subject Nadharia
dc.title Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
NEEMA TANDIKO.pdf 1.169Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account