COSTECH Integrated Repository

Usawiri wa mwanamke katika filamu za kibongo: mifano kutoka filamu teule za Steven Kanumba

Show simple item record

dc.creator Rugamba, Evangelina
dc.date 2019-08-20T07:07:20Z
dc.date 2019-08-20T07:07:20Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Rugamba, E. (2015). Usawiri wa mwanamke katika filamu za kibongo: mifano kutoka filamu teule za Steven Kanumba. Dodoma: Chuo kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/980
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/980
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usawiri wa mwanamke katika filamu za Kibongo kwa kujiegemeza katika filamu teule za Steven Kanumba. Nadharia ya Ufeministi ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data wa tasnifu hii. Data zilikusanywa ni pamoja na filamu teule mbili za Steven Kanumba. Filamu hizo zilitazamwa na kuchambuliwa ili kupata umaizi wa usawiri wa mwanamke. Vilevile, makala, vitabu na tasnifu mbalimbali vilisomwa ili kuona ni kwa namna gani mwanamke amesawiriwa. Utafiti huu umebaini kuwa katika filamu za Kibongo, mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali kama vile mama, mtoto, kijakazi, mwalimu, mzimu pamoja na kahaba. Vile vile, utafiti huu umebaini kuwa jamii inamchukulia mwanamke katika mtazamo hasi. Mtazamo huo wa jamii juu ya mwanamke ni pamoja na vipigo na manyanyaso, kiumbe cha kustarehesha ulimwengu, malaya na muasi wa maadili, kiumbe dhaifu pamoja na kuzalishwa na kutelekezwa. Utafiti huu umebainisha dhamira mbalimbali zilizojitokeza kuhusu usawiri wa mwanamke dhamira hizo zimejitokeza katika pande mbili. Kwa upande wa kwanza dhamira hizo zimejitokeza katika hali chanya kama vile ujasiri na uvumilivu malezi, usiri na staha kwa mwanamke pamoja na misimamo katika maisha. Pia utafiti huu umebinisha dhamira zinazomsawiri mwanamke katika hali hasi kama vile ukatili, unafiki na usaliti, utovu wa maadili pamoja na ushirikina. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Usawiri
dc.subject Wanawake
dc.subject Filamu
dc.subject Filamu za kibongo
dc.subject Ufeministi
dc.subject Steven Kanumba
dc.title Usawiri wa mwanamke katika filamu za kibongo: mifano kutoka filamu teule za Steven Kanumba
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
EVANGELINA RUGAMBA.pdf 645.6Kb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account