COSTECH Integrated Repository

Fani ya methali za kisukuma katika uadilishaji wa watoto na vijana

Show simple item record

dc.creator Raphael, Sostenes Mashinji
dc.date 2019-08-20T08:58:30Z
dc.date 2019-08-20T08:58:30Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:36Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:36Z
dc.identifier Raphael, S. M. (2015). Fani ya methali za kisukuma katika uadilishaji wa watoto na vijana. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/992
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/992
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa fani katika methali za Kisukuma katika uadilishaji wa watoto na vijana. Vipengele vya kifani vilivyochunguzwa na kuchambuliwa ni matumizi ya lugha, wahusika na mandhari. Vipengele hivyo vilichunguzwa kwa lengo la kubainisha namna mfungamano wake unavyochangia kuibua maudhui ambayo hukamilisha tendo zima la kiusemi na namna nguvu ya tendo kusudiwa inavyopokewa na watoto na vijana. Nadharia ya Tendo la Kiusemi (TELAKI) imetumika kuchanganulia vipengele hivyo. Na nadharia ya tafsiri baina ya tamaduni mbili imetumika kwa ajili ya kutafsiri methali za Kisukuma kwa Kiswahili. Katika utafiti huu, jamii ya watafitiwa ilikuwa ni Wasukuma waishio katika maeneo ya mkoa wa Mwanza. Mbinu ya sampuli ya kitabaka ilitumika kuwapata watoto na vijana na sampuli lengwa kwa wazazi na walezi kutokana na tajiriba waliyo nayo katika matumizi ya methali. Ukusanyaji wa data ulihusisha data za uwandani na maktabani. Data zilichanganuliwa kwa njia ya mahojiano na majadiliano baina ya watafitiwa wa makundi yaliyolengwa na kuwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa maadili yaliyomo katika methali za Kisukuma yanatokana na ufungamanifu uliopo kati ya lugha, wahusika na mandhari iliyotumika kuijenga fani ya methali husika. Vipengele hivyo vya kifani ndivyo hubeba matendo kusudiwa yenye ujumbe wa aina mbalimbali unaolenga kuwajengea watoto na vijana maadili faafu katika jamii. Utafiti ulibaini pia kuwa vipengele hivyo vya fani, kwa baadhi ya methali, hutoa changamoto kwa watoto na vijana katika kuuelewa ujumbe uliokusudiwa.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Fani
dc.subject Methali
dc.subject Methali za kisukuma
dc.subject Uadilishaji
dc.subject Watoto
dc.subject Vijana
dc.title Fani ya methali za kisukuma katika uadilishaji wa watoto na vijana
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
SOSTENES MASHINJI RAPHAEL.pdf 2.452Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account