COSTECH Integrated Repository

Utani katika sherehe za harusi za watumbatu: aina, sababu na taashira zake

Show simple item record

dc.creator Gora, Simba Haji
dc.date 2019-08-20T09:17:44Z
dc.date 2019-08-20T09:17:44Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:36Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:36Z
dc.identifier Gora, S. H. (2015). Utani katika sherehe za harusi za watumbatu: aina, sababu na taashira zake. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/997
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/997
dc.description Tasinifu (Shahada ya Uzamili Sayansi ya jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulichunguza utani katika sherehe za harusi za Watumbatu. Utani ni chombo muhimu kinachowasilisha fikira, ujumbe na mwelekeo wa kijamii. Kwa kutumia utani jamii hutambulisha asili, utamaduni wake pamoja na kurithisha mila na silka za jamii. Watani hutupiana maneno yenye mzaha, kejeli, izara na hata matusi makali bila kuzingatia wale wanaowasikiliza, jambo ambalo baadhi ya hadhira hulalamikia jambo hilo. Utafiti huu ulifanyika katika kisiwa cha Tumbatu chenye shehia tatu ambazo ni Uvivini, Jongowe na Gomani. Watafitiwa walikuwa hamsini na watano (55).Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni udurusu, mahojiano, udodoshaji na ushuhudiaji. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Uhemenitiki ambayo inaongozwa na msingi wa kufasiri matini kwa kuzingatia utukuzaji na ufufuaji wa maana za matini kimuktadha, kisaikolojia na kisarufi. Hivyo taashira zilizomo ndani ya utani ziligunduliwa kupitia misingi ya nadharia hii. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwapo kwa aina nne za utani ufanyikao katika sherehe za Watumbatu. Nazo ni utani wa binamu, utani wa mashemeji, utani wa babu/ bibi na wajukuu, na utani wa marafiki. Utani huo hufanywa kwa sababu ya kujitambulisha, kuonesha mahusiano, kufunza na kuburudisha. Aghalabu, utani huo ufanyikao katika sherehe za harusi hutamalakiwa na matumizi ya matusi na kejeli ambazo huwa na taashira maalumu iliyokusudiwa.Pia, utafiti uligundua na kubainisha taashira mbalimbali zinazotokana na utani kupitia maneno na matendo. Hii ni kwa sababu hutoa ujumbe maalumu unaopaswa kuzingatiwa na wanandoa na hata hadhira shiriki wa harusi hiyo. Hii ina maana kuwa utani una nafasi muhimu katika jamii.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Utani
dc.subject Sherehe
dc.subject Sherehe za harusi
dc.subject Harusi
dc.subject Watumbatu
dc.subject Harusi za watumbatu
dc.title Utani katika sherehe za harusi za watumbatu: aina, sababu na taashira zake
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
SIMBA HAJI GORA.pdf 1.333Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account