Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu ulichunguza dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa, uliongozwa na malengo matatu ambayo ni: kuchunguza namna taswira zinavyojitokeza katika nahau za Kisambaa, kuchunguza athari zinazojitokeza katika matumizi ya taswira katika kufafanua na uelewekaji wa nahau za Kisambaa kwa hadhira pamoja na kutathimini uhusiano uliopo baina ya taswira zipatikanazo katika nahau za Kisambaa na maisha halisi ya jamii. Mapengo yaliyojitokeza katika kutoa msukumo wa kufanya utafiti huu ni haya; Kwanza, wengi wa wataalam hao wamezishughulikia nahau kwa kuzikusanya na kuangalia maudhui yake kama walivyotajwa katika usuli wa tatizo la utafiti, hata hivyo, hawakukishughulikia kipengele cha taswira. Pili, uchunguzi wao umejigeza katika nahau za Kiswahili na lugha nyingine lakini sio lugha ya Kisambaa. Mbinu ya udodosaji, mahojiano na mjadala wa vikundi zilitumika katika kukusanya data. Mbinu ya ufafanuzi ilitumika ambapo mkabala wa Umuundoleo ulitumika katika uchambuzi wa data.Vitongoji vitatu pamoja na Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa vilihusishwa katika kuwakilisha watafitiwa. Matokeo ya utafiti yanabaini kuwa nahau za Kisambaa zimeenea katika vipengele mbalimbali vya maisha ya jamii hiyo. Nahau zilizochambuliwa zinaakisi mazingira yanayoihusu jamii hiyo pamoja na vitu vitumikavyo katika jamii husika. Mchango mpya ambao umeibuliwa katika utafiti huu ni kukuza ufahamu juu ya matumizi ya taswira katika Fasihi, hususani katika kipengele cha fani ambapo taswira chomozi katika nahau za kisambaa zimeelezwa kama sehemu ya taaluma katika Fasihi simulizi ya Kiswahili.

Keywords
Dhima, Taswira, Dhima ya taswira, Nahau, Nahau za Kisambaa, Kisambaa, Fani, Semi, Nadharia