Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa

dc.creatorTandiko, Neema
dc.date2019-08-20T06:19:21Z
dc.date2019-08-20T06:19:21Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:35Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:35Z
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionUtafiti huu ulichunguza dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa, uliongozwa na malengo matatu ambayo ni: kuchunguza namna taswira zinavyojitokeza katika nahau za Kisambaa, kuchunguza athari zinazojitokeza katika matumizi ya taswira katika kufafanua na uelewekaji wa nahau za Kisambaa kwa hadhira pamoja na kutathimini uhusiano uliopo baina ya taswira zipatikanazo katika nahau za Kisambaa na maisha halisi ya jamii. Mapengo yaliyojitokeza katika kutoa msukumo wa kufanya utafiti huu ni haya; Kwanza, wengi wa wataalam hao wamezishughulikia nahau kwa kuzikusanya na kuangalia maudhui yake kama walivyotajwa katika usuli wa tatizo la utafiti, hata hivyo, hawakukishughulikia kipengele cha taswira. Pili, uchunguzi wao umejigeza katika nahau za Kiswahili na lugha nyingine lakini sio lugha ya Kisambaa. Mbinu ya udodosaji, mahojiano na mjadala wa vikundi zilitumika katika kukusanya data. Mbinu ya ufafanuzi ilitumika ambapo mkabala wa Umuundoleo ulitumika katika uchambuzi wa data.Vitongoji vitatu pamoja na Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa vilihusishwa katika kuwakilisha watafitiwa. Matokeo ya utafiti yanabaini kuwa nahau za Kisambaa zimeenea katika vipengele mbalimbali vya maisha ya jamii hiyo. Nahau zilizochambuliwa zinaakisi mazingira yanayoihusu jamii hiyo pamoja na vitu vitumikavyo katika jamii husika. Mchango mpya ambao umeibuliwa katika utafiti huu ni kukuza ufahamu juu ya matumizi ya taswira katika Fasihi, hususani katika kipengele cha fani ambapo taswira chomozi katika nahau za kisambaa zimeelezwa kama sehemu ya taaluma katika Fasihi simulizi ya Kiswahili.
dc.identifierTandiko, N. (2015). Dhima ya taswira katika nahau za Kisambaa. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/970
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/970
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectDhima
dc.subjectTaswira
dc.subjectDhima ya taswira
dc.subjectNahau
dc.subjectNahau za Kisambaa
dc.subjectKisambaa
dc.subjectFani
dc.subjectSemi
dc.subjectNadharia
dc.titleDhima ya taswira katika nahau za Kisambaa
dc.typeDissertation

Files