Upande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Tasnifu hii ililenga kuchunguza Upande wa Pili wa Riwaya teule za Shafi Adam Shafi” kwa kuangalia dhamira zilizofichama. Utafiti uliofaywa uliongozwa na malengo matatu ambayo ni: Kuchunguza upande wa pili wa riwaya teule za Shafi A. Shafi kwa kuangalia dhamira zilizofichama katika kazi hizo; Kuchunguza na kubainisha miktadha mbalimbali iliyomsukuma Shafi A. Shafi kutumia mtindo huo katika kazi zake hizo; na Kubainisha athari za mtindo uliotumika katika kazi za Shafi A. Shafi kwa wasomaji wake. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni udurusu wa maktaba, usaili na mahojiano ili kupata taarifa juu ya dhamira zilizofichama katika riwaya. Nadharia zilizotumika katika utafiti huu wakati wa ukusanyaji na uchambuzi wa data ni nadharia ya U-muundo na Umarx. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yalionesha dhamira zilizofichama katika kazi teule kama zifuatazo: harakati za kupigania uhuru kuwa ngumu kutokana na vibaraka vya kikoloni kufaidika na utawala huo, ushiriki wa wasomi katika harakati za kupigania uhuru huo, kusalitiwa kwa wasomi baada ya kupatikana kwa uhuru huo pamoja na suala la ukweli kuhusu harakati za mapinduzi ya Zanzibar. Kutokana na matokeo haya, utafiti huu unashauri mambo yafuatayo: kwanza ni kuzisoma kazi hizi kwa makini ili kuweza kubaini kwa kina juu ya mambo yaliyofichama katika kazi hizi. Pili kazi hizi huweza kutumika kama rejea katika kuijua historia ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Keywords
Riwaya, Riwaya za Shafi Adam Shafi, Shafi Adam Shafi, Dhamira, U-muundo, Umarx, Mitindo