Upande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama

dc.creatorHaji, Gora Akida
dc.date2019-08-28T09:24:16Z
dc.date2019-08-28T09:24:16Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:34Z
dc.descriptionTasnifu (MA Kiswahili)
dc.descriptionTasnifu hii ililenga kuchunguza Upande wa Pili wa Riwaya teule za Shafi Adam Shafi” kwa kuangalia dhamira zilizofichama. Utafiti uliofaywa uliongozwa na malengo matatu ambayo ni: Kuchunguza upande wa pili wa riwaya teule za Shafi A. Shafi kwa kuangalia dhamira zilizofichama katika kazi hizo; Kuchunguza na kubainisha miktadha mbalimbali iliyomsukuma Shafi A. Shafi kutumia mtindo huo katika kazi zake hizo; na Kubainisha athari za mtindo uliotumika katika kazi za Shafi A. Shafi kwa wasomaji wake. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni udurusu wa maktaba, usaili na mahojiano ili kupata taarifa juu ya dhamira zilizofichama katika riwaya. Nadharia zilizotumika katika utafiti huu wakati wa ukusanyaji na uchambuzi wa data ni nadharia ya U-muundo na Umarx. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yalionesha dhamira zilizofichama katika kazi teule kama zifuatazo: harakati za kupigania uhuru kuwa ngumu kutokana na vibaraka vya kikoloni kufaidika na utawala huo, ushiriki wa wasomi katika harakati za kupigania uhuru huo, kusalitiwa kwa wasomi baada ya kupatikana kwa uhuru huo pamoja na suala la ukweli kuhusu harakati za mapinduzi ya Zanzibar. Kutokana na matokeo haya, utafiti huu unashauri mambo yafuatayo: kwanza ni kuzisoma kazi hizi kwa makini ili kuweza kubaini kwa kina juu ya mambo yaliyofichama katika kazi hizi. Pili kazi hizi huweza kutumika kama rejea katika kuijua historia ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
dc.identifierHaji, G. A. (2015). Upande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama.Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1203
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1203
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectRiwaya
dc.subjectRiwaya za Shafi Adam Shafi
dc.subjectShafi Adam Shafi
dc.subjectDhamira
dc.subjectU-muundo
dc.subjectUmarx
dc.subjectMitindo
dc.titleUpande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama
dc.typeDissertation

Files