Uafrikanishaji katika riwaya ya kiswahili
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Description
Ikisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/3160
Makala haya yanajadili namna uchimuzi wa falsafa ya Waafrika unavyochangia kuipa fasihi ya Kiswahili sura ya Uafrika. Vipengele vilivyojadiliwa katika makala hii ni uzazi na ulezi kama jambo la muhimu kwa Waafrika, imani kuhusu uchawi, kuwapo kwa ulimwengu wenye matabaka matatu, mwendelezo wa maisha baada ya kifo na mtazamo kuhusu kuwapo kwa busara na hekima kwa wazee. Swali linaloibuliwa na kujibiwa na makala haya ni kuwa, je, ni kwa namna gani falsafa ya Waafrika imesawiriwa katika fasihi ya Kiswahili, na hivyo, kuifanya kuwa na sura ya Uafrika? Makala yanajibu swali hili kwa mifano hai kutoka katika riwaya za Kiswahili zilizoandikwa kwa kufuata mkondo wa kimajaribio ambazo ni Nagona (1990) ya E. Kezilahabi, Babu Alipofufuka (2001) ya S. AMohammed na Bina – Adamu! (2002) ya K. W. Wamitila.

Keywords
Fasihi, Fasihi kiswahili, Uafrikanishaji, Uzazi, Malezi, Falsafa waafrika, Nagona, Babu alipofufuka, Bina – Adamu