Matumizi ya tamathali za semi katika nyimbo za misiba kwa jamii ya Wahehe

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Description

Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu ulichunguza Matumizi ya Tamathali za Semi Katika Nyimbo za Misiba ya Wahehe. Watafitiwa walikuwa ni Wahehe waishio katika wilaya ya Iringa vijiji vya Tanangozi, Kalenga, Kipera, Mangalali na Nyabula. Jumla ya watafitiwa walikuwa thelathini (30). Njia zilizotumika kukusanyia data ni mahojiano, majadiliano, ushuhudiaji na kurekodi sauti. Data zilikusanywa na kuchambuliwa ili kubainisha ni kwa kiasi gani nyimbo za misiba ya Wahehe zinatumia tamathali za semi, tumeainisha aina za tamathali za semi zinazotumika kwa wingi katika nyimbo za misiba ya Wahehe na tumebainisha dhima ya matumizi ya tamathali za semi katika kuwasilisha maudhui katika nyimbo za misiba ya Wahehe. Data kutoka maktabani zilipatikana kwa kupitia maandiko mbalimbali kufahamu nini wengine wamefanya kuhusu nyimbo za Wahehe. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa njia ya ufafanuzi na data tulizozipata ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Aidha vielelezo vilitumika. Utafiti huu ulimakinikiwa na kuongozwa na mkabala wa Umbuji unaohakiki kazi ya fasihi kwa kuangalia kipengele cha fani na si vipengele vingine.

Keywords

Tamathali za semi, Nyimbo, Nyimbo za misiba, Wahehe, Tanangozi, Kalenga, Kipera, Mangalali, Nyabula

Citation