Matumizi ya tamathali za semi katika nyimbo za misiba kwa jamii ya Wahehe

dc.creatorYangi, Emmanuel
dc.date2019-08-20T06:26:57Z
dc.date2019-08-20T06:26:57Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:34Z
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionUtafiti huu ulichunguza Matumizi ya Tamathali za Semi Katika Nyimbo za Misiba ya Wahehe. Watafitiwa walikuwa ni Wahehe waishio katika wilaya ya Iringa vijiji vya Tanangozi, Kalenga, Kipera, Mangalali na Nyabula. Jumla ya watafitiwa walikuwa thelathini (30). Njia zilizotumika kukusanyia data ni mahojiano, majadiliano, ushuhudiaji na kurekodi sauti. Data zilikusanywa na kuchambuliwa ili kubainisha ni kwa kiasi gani nyimbo za misiba ya Wahehe zinatumia tamathali za semi, tumeainisha aina za tamathali za semi zinazotumika kwa wingi katika nyimbo za misiba ya Wahehe na tumebainisha dhima ya matumizi ya tamathali za semi katika kuwasilisha maudhui katika nyimbo za misiba ya Wahehe. Data kutoka maktabani zilipatikana kwa kupitia maandiko mbalimbali kufahamu nini wengine wamefanya kuhusu nyimbo za Wahehe. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa njia ya ufafanuzi na data tulizozipata ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Aidha vielelezo vilitumika. Utafiti huu ulimakinikiwa na kuongozwa na mkabala wa Umbuji unaohakiki kazi ya fasihi kwa kuangalia kipengele cha fani na si vipengele vingine.
dc.identifierYangi, E., (2015).Matumizi ya tamathali za semi katika nyimbo za misiba kwa jamii ya Wahehe. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/973
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/973
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectTamathali za semi
dc.subjectNyimbo
dc.subjectNyimbo za misiba
dc.subjectWahehe
dc.subjectTanangozi
dc.subjectKalenga
dc.subjectKipera
dc.subjectMangalali
dc.subjectNyabula
dc.titleMatumizi ya tamathali za semi katika nyimbo za misiba kwa jamii ya Wahehe
dc.typeDissertation

Files