Nafasi ya ukristo katika ushairi wa Mnyampala
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili Sayansi Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
Tasnifu hii ilijikita katika kuchunguza nafasi ya Ukristo katika ushairi wa Mnyampala. Mada hii haijawahi kuchunguzwa ingawa wapo waliofanya utafiti wa kazi za mshairi huyu. Eneo la utafiti huu lilijikita katika kubainisha sababu na faida ya Mnyampala kujielekeza katika kuandika mashairi ya dini ya Kikristo. Asilimia kubwa ya utafiti huu ulifanyika maktabani ni kwa sababu taarifa nyingi juu ya Mnyampala zipo katika machapisho aliyoyaandika yeye na kutoka kwa waandishi mbalimbali. Vivyo hivyo mtafiti alikwenda uwandani kukutana na baadhi ya watu waliokuwa karibu na mtafitiwa na waliofanya tafiti juu ya kazi zake. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa, Mnyampala ni mshairi Mkristo aliyekomaa kiimani kutokana na mafundisho ya imani ya kanisa Katoliki.Kutokana na kipaji chake cha ushairi, uamuzi wake wa kutumia ushairi katika kueneza Ukristo ulifata nyayo za washairi kadha waliomtangulia ambao walitumia ushairi kueneza imani zao. Aidha imebainika kuwa mchango wa Mnyampala kishairi umesaidia kukuza taaluma ya ushairi kwa kuongeza maneno mapya yenye dhana ya Ukristo.

Keywords
Ukristo, Dini, Dini ya Kikristo, Ushairi, Ushairi wa Mnyampala, Mnyampala