COSTECH Integrated Repository

Mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili

Show simple item record

dc.creator Kanema, Salum Abdallah
dc.date 2019-08-27T06:45:56Z
dc.date 2019-08-27T06:45:56Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:36Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:36Z
dc.identifier Kanema, S. A., (2015). Mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1105
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1105
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Tasnifu hii, imejikita katika kuangalia na kuchunguza mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili. Tasnifu hii imejielekeza zaidi katika kuangalia na kuchunguza mchango wa kidhamira na kimuundo katika ushairi wa mwandishi huyu. Kuna mchango mkubwa wa ushairi wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili, lakini tafiti na tahakiki za kina hazijafanyika bado juu ya mshairi huyu mwenye ulemavu wa macho. Ingawa tafiti na tahakiki nyingi zimefanywa kuhusu ushairi wa Kiswahili na maisha ya washairi, bado tafiti na tahakiki nyingi hazijamuangalia kwa jicho yakinifu mshairi huyu. Kutokana na hilo, mtafiti wa kazi hii aliona kuna haja ya kufanya utafiti kwa kina zaidi ili kubaini mchango wa mwandishi huyu katika kuendeleza ushairi wa Kiswahili hasa katika kubaini mchango wake wa kidhamira na kimuundo katika ushairi wa Kiswahili. Lakini pia kuna haja ya kujua mbari yake na maisha ya mshairi huyu. Asilimia kubwa ya utafiti huu ulifanyika maktabani na udurusi wa vitabu teule vya mwandishi huyu ambavyo ni Diwani ya Ustadh (1993) na Bahari ya Elimu ya Ushairi (2002). Kadhalika mtafiti pia alikwenda uwandani kukutana na baadhi ya watu wa karibu wa mtafitiwa na kuhojiana na mtafitiwa mwenyewe. Pia, baadhi ya maeneo ikiwemo TATAKI ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilitembelewa ili kupata taarifa zaidi. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa Andanenga ana mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili kidhamira na kimuundo. Kidhamira, yanaonekena mambo mengi yaliyojadiliwa na mshairi huyu katika mashairi yake yanasadifu na kuhalisika katika maisha ya kila siku ya jamii ya Watanzania. Kimuundo, ameweza kubainisha miundo changamani ya ushairi wa Kiswahili na kupata mitindo anuai katika ushairi huu. Ameonesha ustadi wake katika usanaji wa miundo na mitindo ya ushairi wa Kiswahili, ya zamani, ya sasa na mipya hivyo kuupa hadhi ushairi huu.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Andanenga
dc.subject Ushairi
dc.subject Kiswahili
dc.subject Ushairi wa Kiswahili
dc.subject Dhamira ya ushairi
dc.subject Muundo wa ushairi
dc.title Mchango wa Andanenga katika ushairi wa Kiswahili
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
SALUM ABDALLAH KANEMA.pdf 1.493Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account